uscuta

uscuta

Our Music online

tisdag 31 juli 2012

Ukweli wenyewe

Upendo na heshima kwa wanadamu vimekuwa vikipambana mara kwa mara ukizingatia kila mwanadamu ana uwezo na anahitaji heshma ya namna yake.
Imekuwa vigumu kutofautisha kama mwanadamu anachuki au anataka hesma au ana wivu wa kawaida tu.
Tunaona mapambano kati ya Ndugu na ndugu ,Marafiki kwa Marafiki, Mataifa kwa Mataifa n.k
Tumeona swala la Upendo ilikizungumziwa miaka elfu kadhaa ila mpaka sasa mwan...adamu ajaelewa upendo na hesma ni nini.
Ni kweli mtu anaweza kumchukia mwenzie ingawa anampenda?
Je nini kinafanya mtu anakuwa hivyo?
Tumeona tukitofautiana kiimani n.k ,
je ni kweli kwamba chuki inaanzia pale Mwanadamu anapotofautiana?
 
http://www.sanaakennedy.blogspot.se/2012/06/ukweli-wenyewe.html
Wnadamu wamekuwa kwa karibu zaidi kutokana na mfumo wa code.
Wanadamu wamejitahidi kuweka mazingira ya kusaidiana na kuwa kama familia moja.
Hapo zamani ilikuwa vigumu kujenga familia ya mchanganyiko,ilikuwa vigumu kuamuwa kwa pamoja .nk
Kwa sasa tumeona watu wakiwa na lengo moja kutoka pande zote za dunia huku wakijaribu kukutana na kuonyesha kuwa wao ni wamoja.
Dunia inaelekea sehemu ambayo kutakuwa hakuna tena nguvu ya Dini ,rangi wa kabila .
Wnadamu watakuwa kwa pamoja na kushirikiana kwa pamoja.
Kutakuwa na jami kadhaa ambazo zitashikilai misimamo yao ya udini ,urangi n.k lakini hawatakuwa na nguvu kwa sababu jamii kubwa itakuwa inapinga vitu hivyo.
Tatizo kubwa litakuwa ni jinsi ya mwanadamu atakavyojiheshimu na kulinda thamani ya ubinaadamu ambayo amerith tokea kizazi chetu cha kwanza.
Ijulikane kuwa mwanadamu ana tabia moja ,mwanadamu amekuwa akipambana juu ya kuwa na nguvu ili aeshimike kwenye jamii ,iwe inayo mzunguka au Ulimwengu kwa ujumla.
Tumebaguwana kwa rangi na kabila ili iwe rahisi kuwatawala wengine kwa vigezo vya kwamba jamii inayofanana iwe na kiongozi wake.
Dunia ya sasa haizingatii hili ,Dunia ya sasa inazingatia Ukweli,ukweli ambao umezungumziwa tyokea miaka 2000 iliyopita.
Dunia ya sasa imekuwa ikijaribu kuonyesha kuwa inahitaji kuheshimu mazingira na kuona Utu wa mwandamu unathaminiwa.
Ile imani ya watu kadhaa waangamie ili wengine waishi kwa raha imepitwa na wakati.
Dunia ni kijiji na mwanadamu anahitaji kuiona kwa undani zaidi.
Binadamu wamekuwa wakijenga familia kuwa kwenye hiki kijiji tulichonacho kwa sasa,
Mzunguko wa uchumi umeathirika kwa kazsi kwa sababu ya kutokubaliana na hili,
Si kweli kwamba Waafrika wakiheshimika basi uzalishaji wa malighafi utakuwa umepunguwa ,hapana.
Waafrika wanahitaji hesma kama ilivyo kwa mwanadamu yeyote.
Si kweli kwamba Burma wakiheshimika basi uzalishaji wa mpunga utakuwa umepunguwa.
Inaendelea

Inga kommentarer:

Skicka en kommentar