uscuta

uscuta

Our Music online

söndag 6 januari 2013

Nyakati za mampambano

Ninaamuwa kugawa na kutupa vitu vyangu vyote na kuhamia Stockholm.
Mpangilio mzima ulikuwa ni kuhamia kwenye apertment ya mda alafu nitafute yangu ya kudumu baada ya miezi kadhaa.
Ila , safari haikuanza jinsi nilivyopanga nilipofika Stockholm.Ninakutana na vikwazo na ilinibidi nilale kwenye nyumba za kulala wageni.
Naelewa ninachokifanya na ninachokitaka,bali inafikia wakati ninajikuta hela zinaelekea kusiha.Natafuta huku na kule bila ya kupata nafasi ya kulala kwa watanzania wenzangu.
Napata wazo la kwenda Rinkby kwani kule kuna watu wengi wa kutokea Afirka ,naulizia kama wanawajuwa watu wa kutokea Tanzania ,na wananiambia wapo wengi tu.
Napata namba ya simu ya raia wa kutokea Kenya, naamuwa kumpigia ,anapokea simu na tunaanza kuongea.
Namwelezea shida yangu , na ananiahidi kuwatafuta watu wa kitanzania ili awaulizie kama kuna mtu anaweza kunipatia sehemu ya kulala.
Napata wazo , na najiamini kuwa Mungu yupo nami na kama nilipanga kuhamia huku basi nitafanikiwa na haya ni majaribu tu.
Nimekuwa nikiamini kuwa Mungu anatusaidia siku zote tunapokuwa kwenye shida.Tunatakiwa tuwe na imani na kuamini tu.
Inafika usiku wa mwaka mpya ,ninapata ujumbe kuwa kuna mtu anaweza kunisaidia kulala kwa mda wa siku chache.
Tunakutana na ananipa ufunguo wa kwenda kulala kwenye apertment yake.
Tunaenda kuangalia apertment na inabidi nirudi mjini kusheherekea mwaka mpya katikati ya mji wa Stockholm.
Usiku wa mwaka mpya unakuwa ndiyo mpaka wa majaribio mabaya na ni siku nilioombea nchi yangu kuanza kutoka kwenye umaskini.
Nategemea mafanikio makubwa sana mwaka huu na nitawajulisha baada ya kutokea mafanikio hayo.

c Mmbando Kennedy

Inga kommentarer:

Skicka en kommentar