uscuta

uscuta

Our Music online

måndag 22 april 2013

UHUSIANO WA DUNIA YA SASA.

kulikuwa na dada mmoja mwenye kutaka kujenga mpangilio wa maisha yake yawe kwenye mwonekano wa kuendelea na kuwa na uhakika wa kuishi na mwanaume asiye na matatizo yeyote.
Katika kupangilia kwake alikutana na vikwazo vya kupangilia mwenendo wake pamoja na ni mwanaume gani wa kumwamini.
Ni nani adui na nani ni  wa kumwamini ?
Hili limekuwa swali kubwa kwa baadhi ya wanawake walikutana na wanaume mbalimbali na kujikuta wakiwa kwenye mwelekeo usioeleweka kwa kutokana na kutoendana kimawazo na wanaume wao.
Barani Afrika wanawake wamekuwa wakiwaeshimu wanaume wao ila wamekuwa wakijikuta kwenye wimbi la mawazo kwa kuona familia zao zikiwa kwenye wimbi la umaskini pamoja na magonjwa makubwa kama vile ukimwi n.k
Mwanamke amekuwa akihusika zaidi kwenye janga hili haswa kwa kutumiwa na wanaume wasio na huruma na kujali haki za wanawake.
Najuwa inachanganya sana kuelewa na wanaume gani wanaweza kuwa na heshima kwa wanawake ,au kuwajali kuwa na wao wanahitajika kuongoza jamii yetu kwa haki sawa.
Kumekuwa na tabia ya kuwaacha wakina mama wakiwa na watoto wao ,pia kuwabebesha majukumu ya kutafuta chakula pamoja na kulinda familia.
Kwa baadhi ya waafrika wamejitetea kuwa hilo ni jambo la Dini pamoja  mila na desturi.Mimi nadhani ni moja ya kujiteteta kwa kulinda udhaifu.
Kwenye jamii yeyeto ile kumekuwa na kundi la watu wanaojaribu kwenda kinyume cha sheria au misingi waliojiwekea binadamu wenyewe.
Imeonekana kuwa kila mda unapoongezeka Dunia imeingia kwenye majaribio makubwa hasa ya ni hipi baadhi ya vipengele vya haki za binadamu vinaweza kubadilishwa.

Kwakuwa biadamu ni sawa ila wenye siri tofauti na malengo tofauti imekuwa vigumu sana kuweza kuweka misingi ya maisha ya biadamu kwenye usawa.
Kwenye nchi za Ulaya wameweka misingi ya kujaribu kuwaongoza watu kuwajuwa ,kuwapangia watakachofanya na kujaribu kuelezea kuwa wanawapa uhuru wa kuongea.
Mwanzo ilionekana kama ni suluhisho loa matatizo lakini kadri mda unapoenda inaonekana kuwa kama ni      tatizo pia.
Haki za wanawake kuamuwa zimetumika kinyume na kufanya baadhi ya wanaume kuishia kwenye huzuni kubwa kulingana na ushindani uliopo.
Mwanaume anapaswa kuwa na mpangilio mzuri utakaowezesha kupanga maisha yake pia kulinda mfumo mzima wa kazi pamoja na kulelea watoto.
Mwanaume imara amekuwa akijali watoto zaidi na kujaribu kuepukanan na ushindani kutoka kwa mwanamke.
Siku zote kumekuwa na ushindani kwa watu waliokuwa kwenye mahusiano.
Na ushindani umlikuwepo tokea enzi za zamani kwani binadamu na hisia ya kujali sana maslahi yake binafsi.
Katika hisia za mwanadamu kuna jambo ambalo ni lamsingi na jambo hili husababisha hata matatizo makubwa tulionayo kwenye jamii yetu hivi sasa.
Kila mwanadamu anahitaji kuonekaka anafanya vyema hata kama hajuwi.Tunaona hili kwa viongozi wetu mbalimbali kwenye maswala ya uongozi ,pale wanapokuwa wameshindwa na wengine kujaribu kuwarekebisha.
Tendo la kumsaidia binadamu majukumu limekuwa ni kero kwa asilimia kubwa baina ya wanadamu.
Binadamu yeyote ahitaji sana msaada uwe wa kudumu,hii ni pamoja na kusaidiwa kimapenzi.
Familia za sasa zimekuwa zikielekea kwenye kujenga tabia ya kusaidiana kupita kiwango cha kawaida.
Kumekuwa na kundi kubwa la watu wanaoonekana kama wanahitaji msaada ,hii ni msaada wa maisha pamoja hata msaada wa kuangalia familia.
Mzazi yeyote anapenda kuwa na kulinda familia yake.
Tunadhani swala la (kuadopt) linaweza kuwa ni suluhisho lakini si kweli.
Suluhisho la sasa limekuwa ni kupeana mda wa maongezi na kujaribu kujuwana kivipi na ni vipi watu waheshimiane bila ya kujali jinsi ,uwezesho,matakwa n.k
Binadamu wamependa watu ambao hawajali sana hisia ,wamejali kuheshimianan zaidi ya kujuwa undani na matakwa ya mwingine.
Wanawake wanatakiwa kuangalia uhalisi kwa undani na kuepukanan na ndoto zisizo za uhakika  walizonazo.

Hakuna kitu kinachowezekana bila ya kuwa na ujuzi nacho.Haiwezekani kamwe kujuwa mtu mwingine undani wake na dhumuni lake.
Inapaswa kujifunza na kurekebisha zaidi ya kutafuta matatizo zaidi.
Upendo kwa wanadamu ni kitu cha umuhimu kwa kila sehemu
Hii haijalishi jinsia wala rangi ,dini ujuzi n.k
©Mmbando Kennedy 2013
Ukweli wenyewe.

Inga kommentarer:

Skicka en kommentar