uscuta

uscuta

Our Music online

tisdag 11 februari 2014

Usafiri mjini

Tunaamuwa kupanda Garimoshi kuelekea mjini.Kwenye mji kuna usafiri wa treni kwa sababu ya kupunguza msongamano mjini.Baada ya dakika saba wanapanda abiria na safari inaanza.Kunanjia mbili za Garimoshi kukutanisha sehemu nne za mwanzo wa mji.
Huu ni mfano mzuri kwa miji michanga.Muonekano wa mji ni mzuri ila kunatatizo la kusumbuliwa na walevi inapofikia siku za mwisho wa wiki.

Hakuna kizuri kisichokuwa na kasoro.Kuna ukoseaji wa namna fulani ya jinsi walivyotengeneza njia za Garimoshi .
Muundo wake unamapungufu ya kukutanisha miji ya karibu.
Inawagharimu abiria kusafiri mpaka mjini ili kurudi tena kwenye miji iliyokaribu ila inaumbali wa kilomita kama sita tu.

Cha kufanya ni kujenga njia mpya ya kukutanisha miji iliyokaribu .Hii unasaidia kupunguza uaribifu wa mazingira.
Uaribifu wa mazingira ni tatizo kubwa lililoikumba Dunia .Asilimia zaidi ya 80 ya miradi mingi Duniani inahusishwa na uaribifu wa mazingira.
Nimekuwa nikijaribu kushiriki katika kupambana na uaribifu wa mazingira kwa  kiwango cha uwezo wangu.

Inga kommentarer:

Skicka en kommentar