uscuta

uscuta

Our Music online

onsdag 26 mars 2014

Jarida jipya

Nimeamuwa kubadilisha jarida la zamani lenye picha ya sanamu nikiwa ninatengeneza kipindi nikiwa Bagamoyo.Nimeshukuru sana kwa wale wote wliotembelea ukurasa huu kwa jinsi moja ama nyingine.Ninauhakika ninaingia kwenye kipindi cha kutengeneza shule bora ya sanaa kwa ajili ya watu wanyonge wasio na kauili kwenye wingu la watu wasiojali kuwa kuna watu wengine wanahitaji huduma kama wanazopata wao.Sanaa yangu inauwiano na jinsi Baba wa taifa la Tanzania Mwl Juliasi Kmabarage Nyerere alivyokuwa anatusii tusishi kama raia wema wa Taifa la Tanzania.
Najuwa inakuwa vigumu kwa watu wengine kuelewa kwa uwa wana wingu la hofu ya kutofanikiwa ikiwa hawatawatenga watu wengine na kujikweza kwenye mambo mbali mbali.Tunajuwa kuwa sanaa ni chombo imara chenye kuweza kuwabadilisha watu wakawa wamoja kwa mda mfupi.Sanaa imechukuwa nafasi kubwa kwenye mabadiliko ya jamii na inaendelea kutoa nguvu kwa baadhi ya watu wanaoijuwa na kuitumia.
Kuna tofauti kwenye jarida lililopita na hili jipya ninaloweka.Ni kazi kwenu kusoma na kugunduwa kinachofuatia kwa kuangalia jinsi lugha ya hayo majarida mawili ilivyotumika.
Jarida la kwanza.

.....................................................................................................................................................
Kila mtu anapitia njia mbali mbali ili kujifunza jinsi ya kutatawala maisha yake mwenyewe.Kuna njia nyingi za kutawala maisha uluyo nayo ikiwa ni pamoja na jinsi ya kujenga urafiki , kumaliza urafiki ,kujenga uchumi na kuulinda pamoja na mambo mengi tu.
kuna joinsi watu wengine watakavyokufikiria na kujadili juu yako ingawa njia bora ni kuwaweka mbali na kujilinda kwa kila utakavyo weza.
Baadhi ya watu wanatumia njia ya kujidai hawaongei wakati unakuwa nao ili waweze kuchukuwa yale uliyo nayo .Njia moja ya kuwa tega ni kuongea zaidi na kutumia njia potofu ili uwapime wanaupeo gani wa kungamuwa.
Baada ya muda utagunduwa kuwa wanarudia yale uliyosema ili wakuonyeshe wanakuelewa.Baada ya mda wanaanza kujenga urafiki kati yao ndani yako ili waweze kukushambulia.
Utakachofanya ni kuwasoma bila ya wao wenyewe kungamuwa na kujifanya mjinga kwa yale wao wanayofikiria ni muhimu kwenye maisha.
Mambo mengi wanayofikiria ni muhimu ni pamoja na uchumi wa fedha ,kukaa kimya wakati wa mazungumzo n.k
Unapaswa uzungumzie maswala ya uchumi kwenye njia rahisi ili wao wajuwe kuwa hauelewi kiundani uchumi kama wao wanavyoelewa.
Baada ya mda ni kuanza kufuta uhusiano wa urafiki na yeyote atakaye onyesha kuto kukujali.
 
Mwanzoni watazani umeshindwa kwani wanakila kitu unachojuwa wewe na baada ya mda watagunduwa hawana kila kitu unachojuwa wewe kwani hawakuwa na cha kukupa wewe na wewe umewapa kile kidogo kinacho wafaa.

Mmbando kennedys JF Drawing.

Inga kommentarer:

Skicka en kommentar