uscuta

uscuta

Our Music online

torsdag 6 mars 2014

Kijana na ujenzi.

Ikawa usiku kwenye giza nene .Kulikuwa na kundi la walioamini na wasio amini .Walijaribu kumshirikisha kijana yule kwenye mawazo ya miradi yao.Walipanga kujipaka mafuta ikiwa ni kinga ya kupambana na nguvu zote za giza .Walijikuta hawajajiapa na yule kijana alikuwa amepakwa mafuta mwili mzina .Walijaribu kwa silaa za aina mbalimbali na ilionyesha kuwa hakuna silaa inayoweza kumgusa kijana yule.
Mo...ja ya hao watu alijivalisha sura ya rafiki wa yule kijana na kuanza kumjaribu yule kijana kwa kusema:
Mbona una bunduki mkononi?
Yule kijana akajibu :
Hii si bunduki ni silaa kali yenye mfano wa silaa zote unazozijuwa.
Mzazi wa yule kijana mwenye damu ya kiongozi fulani alianza kwa kumpa yule kijana kazi ya kulinda wananchi na mali zao.
Alianza kwa kukejeli :
-Naona tupo benki na kunawatu wamepanga uvamizi .Unawezaje kutumia silaa yako ikiwa una bunduki ambayo haijajazwa risasi?
Kijana hakumjibu.

Cha kushangaza yule mtoto wa mkubwa alianza kukimbia upande wa pili na kuonyesha kidole kwa wale waliokuwa karibu na jengo kwa kusema tumempa kazi ya ulinzi yule kijana pale.
Ghafla akajitokeza mwingine aliyevaa umbo la rafiki wa yule kijana ambaye ni mchezaji mpira.
Alimuuliza kijana:
-Ni nani amekupa hii kazi kwani hata mimi ningependa kuifanya.
Kijana alijitaidi kumfundisha lakini yule mcheza mpira hakuelewa.
Ghafla ikatokea shindano la kucheza mpira.

Ilikuwa hivi mchezaji bora anatakiwa apige mpira eneo la 18 nje kidogo ya goli .Mshindi ni yule atakaye piga mpira na ukawagusa wachezaji wote walikuwa karibu na goli.
Ni mmoja tu kati ya waliopiga alifanikiwa kugusa watu wanne ingawa mcheza mpira alishindwa kabisa, aligusa mmoja au wawili.
Ikafikia zamu ya kijana kupiga mpira.
Mwamuzi alimwangalia yule kijana kwa jinsi alivyo kaa na kumwambia ameona mpira wake utagusa watu wengi na ni bora asishiriki kupiga.

Mcheza mpira alijaribu kumuuliza kijana mbinu za kuweza kupata ajira na inakuwaje akaweza kucheza mpira akiwa si mchezaji.
Kijana alimfundisha ila mcheza mpira akuelewa.
Ghafla walitokea sehemu nyingine yenye watu wa aina mbali mbali kulikuwa na nyumba ikijengwa ni nyumba ya kawaida isiyo malizika.
Wajenzi walikuwa na vifaa vya kila aina ,walionekana kuijenga kwa kasi.Walipanga matofali usiku kucha lakini hawakuimaliza ile nyumba.Ulikuwa ujenzi wa zaidi ya miaka mia moja.
Mcheza mpira aliwashauri wa mwajiri yule kijana kwani alikuwa amepakwa mafuta mwili mzima na ilikuwa vigumu kuathirika na saruji .
Mcheza mpira aliwashauri hivyo kutokana na watu wengi kuathirika na Saruji.
Walionekana wakiwa wamekatika na saruji wanayoibeba usiku kucha.
Ghafla alitokea kiongozi mwenyewe na kusimama mbele ya yule kijana.
Kijana alimpika kiongozi kifuana na kumweleza hivi ndiyo tunatakiwa kujenga nyumba.
Kiongozi alifurahi na kumwelezea kijana jinsi alivyoanza ujenzi wa nyumba ile.
Kijana alielewa na kuona lengo la yule kiongozi na jinsi yeye atakavyoshiriki.
Ikawa zamu ya kuangalia uhalali wa kuwa mwanadamu....................................................................

Inga kommentarer:

Skicka en kommentar