MGAWANYO WA UWASILISHAJI MAWAZO.

Dunia imekuwa ikipigania haki ambayo inasemekana inatokana na usawa wa kidemokrasia.
Kuna mambo mengi ya kufuatialia kwenye demokrasia ya nchi yeyote japokuwa la umuhimu ni kujuwa sheria na haki za binadamu ya nchi husika.

Haki ya binadamu ni nini?

HISTORIA NA MATUKIO YA HAKI YA MWANADAMU KABLA YA ZAMA ZA CHUMA.
Kumekuwa na mvutano mkubwa wa  jinsi gani watu wanadhani ni haki kwa mtazamo wao.
Haki za binadamu zimejengwa kwenye vipindi tofauti hapa duniani.
Muundo wa kwanza wa haki za binadamu ulijengeka kwa mahitaji muhimu ya kwanza ya binadamu na mila na desturi zao za awali zilizolinda matakwa ya dini au imani waliyo nayo.
Kulikuwa na jamii ndogo ndogo na zilikuwa zinatambuwa na kuelewa mazingira yaliyowazunguka.Jamii ya awali ilitambuwa tabia ya mgeni yeyote aliyeingia kwenye jamii yao.
Ili mgeni akikubalike ni lazma ajitambulishe kwenye jamii husika na kuieleza ni nini kilichomfanya awepo mahala pale.
Kwenye nchi za magharibi kulikuwa na tabia ya kujenga ukuta mkubwa wa mawe na kila ndani ya jamii husika kulikuwa na mfalme.Jamii ilijenga jeshi dogo ili kujilinda na uvamizi kutoka jamii nyingine ,ingawa kila jamii ilivutiwa tu na yale waliyokuwa wanafanya wenyewe hawakuwa na haja ya kujuwa ya wageni.
Katika kila bara kulikuwa na jamii ya wafugaji na wavuvi ambao wao walikuwa wanahamahama.Jamii ya wavuvi ya nchi za magharibi VIKING  ,jamii ya wafugaji barani Afrika Wanubia ,Wahabesh ,Wamasai ,wawindaji reds Indians ,wafugaji wa nchi za Norway na Sweden Sormanar ,Wayahudi , Wazuru n.k
Jamii hizi zilianza kujichanganya na jamii mbalimbali pindi zilipokuwa zina hamahama.Baadhi yao walikuwa wakivamia jamii nyingine na kwa lengo la kuchukuwa kila walichokuwa na nao.
Katika vitu walivyokuwa wakinyanganya ni chakula ,Vito vya madini kama dhahabu ,walichukuwa wanawake n.k baadhi ya makundi yalitambulika kwenye karne ya 19th mengine yalikuwa kabla ya Yesu kuzaliwa  soma # Egypt: Nubia #Vikingar #Jewish history

KUENEZWA KWA DINI NA KUPOTEA KWA MWONGOZO WA HAKI ZA BINADAMU ZENYE MLENGO WA KIAFRIKA.
Kulikuwa na uenezaji wa dini kuu mbili ya kikristo na kiislamu kwenye miaka miatano baada ya kuzaliwa Yesu.
Jamii mbalimbali zilivutiwa na moja ya dini hizo mbili kwa kusoma na kufuata yale yaliyoandikwa na wasomi wa dini hizo.
Jamii hizo zilianza kukuwa na kujikuta zimejenga makundi mawili makubwa ikiwa moja ni la kiislamu na moja ni la kikristo.Jamii iliamini ili kuwa mwanadamu kamili na mwenye kufanya mambo mema lazma uwe muumini wa moja ya dini hizo.
Kulikuwa na mgogoro mkubwa wa ni dini ipi halali. Waumini wa dini hizi mbili wamekuwa kwenye upinzani mkubwa wa ni yupi ana dili halali na imesababisha nchi nyingi kuwa kwenye matatizo ya ni jinsi gani jamii inaweza kueshimiana kutokana na utofauti wa dini hizi mbili.
Kwenye kipindi cha kueneza dini kulikuwa na biasha kubwa ya watumwa kwenye bara la Afrika.
Wakoloni wa kwanza walitokea nchi za Uarabuni mfano Oman ,Saudiarabi n.k
Wakoloni wa pili walitokea nchi za ulaya ,Ujerumani ,UK Uingereza ,Ufaransa ,Ubeligiji,Ureno n.k
Baadhi ya watemi wa kiafrika waliamuwa kushirikiana na wakoloni huku wengine wakiingia kwenye vita kali ili kulinda jamii yao isichukuliwe utumwani kwenye nchi za magharibi ,asia na Amerika.
Lengo la nchi za magharibi ilikuwa ni kuanzisha kilimo katika nchi ya Amerika kaskazini haswa USA na walikuwa bado hawajangunduwa mashine za kufanyia kazi hivyo waafrika ndiyo walionekana kuwa wanavumilia kufanyishwa kazi ngumu.
Soma # Tippu Tip 1837 - 1905
Kwa nchi za uarabuni waliamini wanahitaji watu wakuwasaidia kazi na waafrika ndiyo walikuwa moja wa vitendea kazi vyao kutokana na imani waliyokuwa nayo.
Katika kipindi hiki waafrika wengi walikosa haki za kimsingi za uanadamu .
Waafrika walijiona wanahadhi pindi wanaposali pamoja na moja la kundi la Wazungu au Waarabu.Watu wa kawaida hawakuwa na uwezo wa kushiriki kwenye sehemu hizo bila ya kukubaliana na matakwa ya hao Wazungu na Waarabu.
Kwa hiyo haki zote za bianadamu zilielemea kwenye matakwa ya Wazungu na Waarabu.Waafrika wengi walisaau mila na desturi zao na kujikuta wakijifunza zile za wageni.
Wazungu na waarabu walitofautiana kwenye haki za binadamu ingawa waliamuwa kufanya kazi kwa pamoja na kutoingiliana kwenye makoloni.
Ethiopia ilikuwa ni nchi pekee iliyo athirika kidogo na mabadiliko haya kutokana na kutotawaliwa.
Wakati Bob Malrey akiwa kwenye kuelewesha jinsi waafrika wangeweza kuwa pamoja na kuwa Huru .

AFRIKA IMEKOSA MPANGILIO MZIMA WA JINSI GANI JAMII INAWEZA KUSIKILIZANA NA KUAMUWA MAMBO KWA PAMOJA.
Baada ya nchi za magharibi na za uarabuni kuweza kuitawala Afrika walijikuta wakiigawanya Afrika kwenye makundi mbali mbali ya jinsi ya kufikiri na uwezo wa elimu ya kijamii.
Kundi la kwanza lilikuwa la Afrika magharibi ambalo lilikuwa na nchi zilizo tawaliwa na Ufaransa na kupewa nafasi ya kushiriki kwenye vita ya dunia.Kundi hili lilikuwa na watu wenye uwezo wa kufikiri na kuamuwa mambo kwa asili ya kifaransa.
Kundi la pili ni la Africans Amerika ambao waliamuwa kutafuta jinsi ya kurudi nyumbani baada ya kugunduwa wana haki na walishajifunza na kuelewa jinsi ya kuwasiliana na kupambana na mabavu ya nchi za magharibi.Kundi hili lilisafiri kwenye nchi za Amerika ya kusini na kundi moja lilifanikiwa kuwasili Afrika. Soma maisha ya # marcus garvey  marcus garvey
Kundi la tatu lilielewa mila na desturi za kiarabu na kuamuwa kuanza kufanya biashara na kushirikiana kwenye baadhi ya mambo.Kundi hili ni la nchi za kaskazini na pamoja na baadhi ya nchi za magharibu mfano wa nchi za magharibi ni Mali  mfano wa nchi za kaskazini  Misri,Sudani ,Libya n.k Nchi hizi zimekuwa zikipambana kutokomeza kabisa mila na desturi za watu wa magharibi na kuahakikisha wanatokomeza pia imani ya kikristo.
Kundi jingine ni la nchi za Afrka mashariki na kati na kusini ambazo ni Kenya ,Tanzania ,Uganda ,Msumbiji, Afrika kusini ,Kongo ,Zambia ,Zimbabwe ,Rwanda ,Burundi,Visiwa vya shelisheli ,Madagaska n.k
Baadhi ya nchi hizi zimeingiliana kwenye mila na desturi ingawa baadhi ya nchi zinawakoloni tofauti.
Nchi zilizokaribia na magharibi zina watu wenye mlengo wa nchi za Ufaransa na Uberigiji wakati nchi za mashariki ukiondowa Msumbiji ambao walitawaliwa na Wareno wengine wana mlengo wa Uingereza na Ujerumani.
Kumekuwa na tatizo kubwa zaidi kwenye ´nchi za Afrika mashariki na kusini  kwani nchi hizi zina mchanganyo wa mila na desturi za kiarabu na Kizungu huku nchi ya Afrika kusini ikiwa inautamaduni mkubwa wa nchi za Ulaya kwa kuwa walipata uhuru mda si mrefu.

DEMOKRASIA YA BARA LA ULAYA IMEJENGWA MIAKA NA MIAKA KWA MATUKIO MBALI MBALI IKIWEMO VITA YA KWANZA NA YA PILI YA DUNIA.


Entente and Allies (some entered the war or dropped out later)
Neutral Countries

Kabla ya kuendelea angalia picha kwa umakini na tambua muundo mzima wa Vita ya kwanza  dunia ulivyokuwa umepangwa.

Nchi nyingi za ulaya zimekuwa zikitenda haki kwa raia wake si kwamba zinamiujiza ni kwa jinsi walivyojijenga na kutambuwa jinsi ya mawasiliano yao na ni jinsi gani wakubaliane kwenye uamuzi wa mambo yanayohusu jamii yao iwe magumu au marahisi watakubaliana kwa pamoja na kufanya uamuzi.
Napenda niishie hapo naweza kuchambuwa muundo mzima kwa muonekano tofauti na nimeamuwa kupitia juu mtazamo huu  tu na nategemea kuandika zaidi ili tukumbuke na kujitambuwa tulipotokea.
.Cha muhimu ni kujifunza na kuheshimu mawazo ya mwenzio na kujaribu kuyafanyia kazi ,kama hayana umuhimu ni bora kuyaacha bila kupingana na kama yanamapungufu ni bora kuyaboresha .
Kumekuwa na watu wanavamia mitandao na kuanza kuwahukkumu wenzao ,Mfano Angalia nadai nchi yangu wewe si mwenzetu , Umeenda shule ,? n.k
Tatizo si nani mjuaji tatazo ni jinsi ya kutatua mzigo huu mkubwa uliokuelemea Mwafrika mwenzangu.
Ok : mnakaribishwa kuchangia , iwe kuongezea kuendeleza kwenye gazeti au redio  kama ni mwandishi ili jamii yote iweze kujadili.
Cha msingi ni kujuwa haki za msingi za bianadamu ni zipi ?
Haki za kawaidi?
Demokrasia katika muundo wa serikali : ambapo kuna demokrasia ya moja kwa moja na ya kushirishwa.

AV Mmbando kennedy
 

Kommentarer

Populära inlägg