uscuta

uscuta

Our Music online

torsdag 7 maj 2015

Mwanaume na mazingira

Najaribu kutoa somo. Unajuwa umuhimu wa Mwanaume kujitambuwa kwenye jamii ni bora kuliko kitu kingine chochote kwenye maisha na utawala wa Dunia? Unajuwa kuwa kila Mwanaume ameumbwa ili kuchukuwa majukumu ya kutawala familia yake pamoja na mazingira yanayowazunguka? Kila mwanaume ni kiongozi. Nimeamuwa kuandika ili kuweka wazi ili kujuwa ni kwa nini jamii imekuwa haijijengi na tumekuwa tukilaumiana kila kukicha kutafuta mchawi. Sasa basi ,kuna kitu kinaitwa utawala wa dunia. Utawala wa dunia alipewa Mwanaume.Na ili kuvuruga dunia ni lazma shatani awe na maajenti wa kuvuruga mpango mzima wa mwanaume. Kitu gani maajenti wanaweza kutumia kufanikisha lengo lao? ni kwa kubadilisha sanaa na kuifanya kuwa ya kishetani.Shetani anaumia sana pindi anapoona mafanikio ya mwanaume pale anapojaribu kuwa na maono na kuongea na mwenyezi Mungu.Kumbuka Historia inasema Eva aliongea moja kwa moja na sheta .Lakini Adamu alishawishiwa na Eva kula tunda la mti wa kati la kujuwa mema na mabaya ambalo Adamu alikatazwa na mwenyezi Mungu. Kwa kusoma mwanzo kwenye biblia utaona Adamu alikuwa anazungumza na moja kwa moja na Mungu .Adamu alikuwa anaishi duniani na alikuwa nauwezo wa kuwasiliana na Peponi moja kwa moja.Kwa hiyo Mwanaume ana uwezo wa kuwasiliana na Mungu moja kwa moja. Tukiacha na hayo ,nimeona niandike ujumbe huu kwani tumekuwa na wasanii wengi haswa wanaume wasiopewa nafasi kwenye ya kuwasiliana na jamii yao kwa sababu sanaa ni moja ya kiungo kinachoweza kubadilisha jamii kwa mda mfupi na sanaa inayotumika mizani yake imeegemea kwenye ushetani zaidi. Hivi karibuni tumeona jinsi wasanii wa Marekani walivyo onyesha nyeti za wake zao adharani huku wengine singel wakisindikiza kwa mbwembwe nderemo na vifio. Hii ni kuonyesha utawala wa Mwanaume unataka kuangushwa na shetani. Kuna watu wanadhani mwanaume kutawala ni kosa . Wengine wamekuja na wazo na feminist huku wakiingiza na maajenti wa Shetani. Kumbuka hamna umuhimu wa maisha pasipo na utawala wa mwanaume. Hii ni elimu ya bure ambayo kila mwanadamu alitakiwa kujuwa.Kumbuka hata katika uumbaji Mungu alimuumba Adam kwanza Kwa mujibu huu mwanaume ndiyo msingi wa familia . Nimebahatika kuona mengi na kujifunza sanaa za watu mbalimbali na kugunduwa sanaa ya nchi zisizoendelea zinabadilishwa ili kuuwa maono ya wasanii wa nchi hizo mfano Tanzania n.k maajent hawa wanatumika kusambaza sanaa za kishetani ili kuuwa mawasiliano ya Mungu na wasanii wa nchi husika. Msanii ni kioo cha jamii ,kweli au si kweli ? Sasa jiulize ni wasanii wangapi wanaweza kuwa kioo cha jamii yetu ya sasa. Kumbuka Tanzania ilitakiwa iwe nchi ya wakulima ,wavuvi na wafugaji. Hamna kitu kitakacho muudhi Mwenyezi Mungu kama cha mwanaume kupoteza mwelekeo na kwenda kinyume na yale ambayo mwenyezi Mungu amepanga.Inga kommentarer:

Skicka en kommentar