uscuta

uscuta

Our Music online

onsdag 1 juli 2015

JINSI YA KUTENGENEZA WAZO LA BIASHARA

Elimu ya biashara  ni kitu muhimu katika nyanja zote za elimu.
Mimi binafsi ni msanii lakini nimewahi kujifunza elimu ya msingi ya biashara.Nilichogunduwa ni kwamba biashara ni mkombozi wa yeyote yule atakayekuwa na mawazo ya mapinduzi ya kiuchumi .Kuna Aina mbalimbali za biashara ila ningependa kuelezea jinsi ya kubuni wazo la biashara kiujumla.

Wazo la biashara ni chombo ambacho kitakusaidia kuanza kampuni (biashara yako) .
Ukiandika vizuri wazo lako litasaidia kuweza kugunduwa haraka lengo la kazi yako.Unatakiwa kufikiria kwa makini kabla ya kuanza biashara yeyote ile.

Vitu vya kuzingatia kabla ya kuanza biashara
1 .Ni bidhaa ipi unataka kuuza
2 .Ni nani atakuwa mnunuzi (Wateja)
3 .Soko la bidhaa hiyo likoje au ni kwa mda gani wateja watakuwa wanategemea kununuwa bidhaa
    hiyo (Zingatia nyakati)

wazo la biashara linatakiwa liwe rahisi kueleweka linatakiwa liwe rahisi kueleweka na liwe kwenye mpangilio halisi pia lenye kuvuta fikra za wateja wako wawe na hamu ya kuona biashara hiyo ikiendelea.
Ila wazo la biasrahisihara linaweza kuwa sana kueleweka au vigumu kutokana na linategemea utendaji wa kazi pale utakapoanza.

Baadhi ya mawzo ya biashara hutegemea bajeti tatu.
1 .Bajeti ya mwanzo
2 .Bajeti ya matokeo
3 . Bajeti ya hali ya kama kimiminiko

Wazo la biashara halihitaji kutokana na utambulisho wako au vitu unavyopenda wewe mfanyabiashara bali linategemea jinsi wateja wako wakilisikia watakuwa na hamu ya kusikiliza au kuona hiyo biashara ikifanyika.

Hitimisho
Hayo ni machache ambayo ninayajuwa kuhusu kutengeneza wazo la biashara ila ni vizuri nikimalizia na kudokeza kidogo tu vitu vya kufanya ili kufunguwa kampuni nayo ni
Mtaji
Kujuwa Aina ya vibali unavyotakiwa kutumia
Kuwa na jengo au ofisi ya kufanyia biashara hii itasaidia wateja wako wakupate kwa urahisi
Linda wazo lako
Funguwa bima yako pamoja na biashara yako
Akhsanteni
Tunaweza kuchangia zaidi ili kuongeza ujuzi haswa kwa wale wadau wa hii fani
Wenu katika ujenzi wa Sanaa
Mmbando Kennedy
Twitter @mmbandoz
Instagram #mmbandokennedy
www.sanaakennedy.blogspot.se
https://www.youtube.com/user/youthvijana
https://www.reverbnation.com/mmbandokennedy
 

Inga kommentarer:

Skicka en kommentar