uscuta

uscuta

Our Music online

måndag 13 februari 2017

Kumekuwa na headsline kwenye moja ya gazeti kubwa nchini Sweden kuhusu sanaa na msanii wa kimataifa kutoka Tanzania Kennedy Mmbando .
Moja ya vitu vilivyozungumziwa ni Historia ya maisha yake kwenye sanaa ,jinsi ya kuwasaidia vijana wasanii ,nguvu iliyopo kwenye sanaa ya msanii ambayo inaonyesha kuwavutia wengi pamoja na lengo la sanaa yake kwa siku za mbeleni.
Mwandishi ameelezea kuwa sanaa ya kennedy inaelezea kwa umakini dhima nzima ya uhamiaji hapa duniani ikiwa ni pamoja na Ongezeko la wakimbizi kutoka barani Afrika huku watu wakiwa na picha ya Waafrika ni watu wa uhalifu.
Makala hii imepokelewa vizuri na jamii ya watu wa hapa na imewajengea shauku ya kujuwa zaidi na kutaka kuwa na mahusiano na nchi ya Tanzania.
Ni matumaini yetu kutakuwa na watalii zaidi kutokea Orebro Sweden mwaka huu 2017.Inga kommentarer:

Skicka en kommentar