Je kuna sanaa ya usasa ktk bara la Afrika

Kumekuwa na maswali yanayotokea mara kwa mara pale inapofikia wasanaii wa Kiafrika wanafanya shughuli zao kwenye nchi za magharibi.
Mara nyingi wahusika wa maswala ya sanaa kweye nchi hizi hujaji kwamba sanaa za kiafrika ni primitiv yaa ni za zama za kale au kizamani.
Wahusika wanaofanya kazi ya kutangaza sanaa za kiafrika wanahitaji kutafuta njia mpya ya kutambulisha sanaa ya kiafrika kama ni ya kisasa kwa aina fulani.
Usasa na ukale ni swala la aina moja tu ila yanatofautiana tu pale wakati muhafaka unapohitajika.
Mfano tunavyoviona ni vya kale sasa vilikuwa vya usasa kipindi kile ,Na tunavyoviona ni vya usasa sasa vitakuwa vya kale hapo mbeleni.
Nimesoma baadhi ya magazeti huku Ulaya ambayo yameanza kuandika habari za wasanii wa Kisasa wa Kiafrika ambao wanadumisha mila na desturi zao huku wakiwakilisha kwa hali ya usasa.

Kommentarer

Populära inlägg