uscuta

uscuta

Our Music online

lördag 1 september 2012

Ukweli wenyewe Na Mmbando Kennedy

Uandishi na ufanyaji wa kazi sanaa umekuwa kama ni kitu cha kila siku katika maisha ya kila siku.
Njia mojawapo nayopenda kutumia ni kusikiliza na kuandika ama kuumba.
Natumia mda mwingi kuisliliza au kuangalia kazi za watu wengine na kulinganiasha na uwezo wangu na hii ndiyo siri kubwa ya mafanikio yangu.
Nimegunduwa kuwa uwezo wa kujuwa ni mzuri kuliko ule uwezo wa kuweza kufanya tu.
Mwanadamu ameweza kufanya mambo mengi lakini kitu kimoja kinazuia ni kuweza kufanya bila kujaribu kujwa vitu vingine ni kuzuia upeo kukuwa.
mfano
kulikuwa na wanafunzi katika makundi mawili, mwalimu aliwagawa ili kuona ni kundi lipi lingefanya kazi kwa uelewa zaidi .Katika kufanya hivyo walipanga kutowa kazi ambayo wanafunzi wote wangeweza kufanya kwenye makundi yao na kurejesha baada ya wiki moja.
Kundi la kwanza lilikuwa ni kundi la wale wanaoelewa zaidi na kundi la pili lilikuwa la wale wasio elewa zaidi.
Kundi la kwanza waliamuwa kuku tana na kujadili jinsi ya kufanya ile kazi na kundi la pili walifanya hivyo hivyo.
Kundi la kwanza waligunduwa kuwa wanawezakufanya kile walichotumwa na mwalimu lakini kundi la pili walikuwa na mtu mmoja tu ambaye anaelewa jinsi ya kufanya vile walivyoagizwa na mwalimu.
Basi kundi la kwanza waliamuwa kukutana siku moja kabla ya kukusanya kazi waliyoagiziwa na mwalimu huku wakijuwa wanaweza kuifanya kwa urahisi kabisa.
Kundi la pili waliamuwa kukutanan kila siku ili wajifunze kutoka kwa yule anayejuwa.
Baada ya kundi la pili kukutana kwa siku tatu mfululizo ndipo waligunduwa kuwa kuwa kile walichofundishwa kilikuwa kinamakosa kadhaa.
Walijadili kwa siku moja zaidi na kugunduwa ni kweli zoezi lilikuwa na makosa.
Huku kundi la kwanza walikutana na kufanya kazi waliyopewa na kukusanya bila kuangalia kama walichozania kilikuwa siyo.
Kundi la pili walielekea kwa mwalimu na kumweleza kuwa waliona makosa kwenye zoezi walilo pewa.
Basi mwalimu aliamuwa kuwapa point za nyongeza wale wanafunzi na ndipo alipo wajulisha wale wanafunzi wa kundi la kwanza kuwa hawakutumia mda kudadisi kile walichopewa kutokana na kujuwa kwamba wanaelewa swali waliloulizwa.
Ni mfano rahisi katika mifano iliyotokea ila inamaana sana kwa watu wasiyofikiria kuwa kuna uwezo wa kutotimiza kile mtu anachokijuwa kama kutakuwa na kukosekana udadisi na ushirikianao wa mtu kwa umakini zaidi.
Itaendelea ,

Inga kommentarer:

Skicka en kommentar