Mwafrika Amka!

Mwafrika Amka.
Imefikia wakati tabaka la Waafrika linazidi kukua.
Waafrika wengi wanabaguana kwa Dini,Siasa,Rangi,kimaisha,uchumi,ukabila  na Mengineyo Mengi tu.
Imekuwa vigumu kwa mtu anayeitwa mwafrika kuepuka migogoro .
Najuwa mila na desturi zetu Waafrika ni Heshma na utii haswa kwa waliotuzidi umri yaani wakubwa zetu.
Wakubwa ndiyo mfano kwa vijana wanaochipukia kwenye jamii yeyote.Ukiona wakubwa hawajiheshimu ujuwe vijana hawatajiheshimu Pia.
Tunaona mijadala mbalimbali ya jamii ambayo inadharauriwa na wasomi wa kiafrika huku ikiwa ndiyo suluhisho la matatizo kwenye jamii.
Kunawasomi wanaoamini kuwa walio chini wawe chini ili wao waendelee kuwa juu.Mimi naamini ni uongo na ninavigezo vingi vya kisayansi vinavyo pingana.Mfano mmoja ni Umbo la dunia,ukihitaji zaidi wasiliana nami.
Dunia inazunguka imefikia mwanadamu anafanya maovu zaidi ya Shehtan.
Dunia inaishi kwa uwiano.Kuna wawakilishi wa kila kinachoonekana humu na visivyoonekana humu Duniani .
Niwaulize swali :
Yupi mwovu kati ya mtuma dhambi na mtenda dhambi?
Nimekuwa na sauti ya jamii yangu tokea nikiwa mdogo.Nimekutana na watu wa aina tofauti ,Waafrika ,Waasia,Wazungu ,Waarabu ,n.k
Nimejifunza na nimefundishwa juu ya kujuwa na kufahamu dhamira za watu mbalimbali .Najuwa ni rahisi kudharau ila si rahisi kusahau.
Nimekutana na watu wengi tu wasio jali wala kutakia mema jamii ya Waafrika .Ninasikia hosianna zao na nafsi zao zikinongona.
Najuwa Asili itawahukumu kutokana na uharibifu walioufanya kwa kipindi hiki tunaishi hapa Duniani.
Imefikia wakati Waafrika tuamke na kujenga jamii yetu kwenye muundo mzuri wa mila na desturi zetu.Tuache kukopi na kulazimishwa kufanya mila na desturi za wakoloni.
Kila siku tunaangalia wao wakiwauwa Manabii na Viongozi tuliopewa na Mwenyezi Mungu? Hivi kunamtu anahitaji elemu ya kujuwa hili?
Mwafrika Amka!

Kommentarer

Populära inlägg