KUMKUNURA MTESA WANADAMU.

Glafla Sofia anafika nyumbani kwao ni mda mrefu alikuwa mbali na mama yake pamoja na kaka yake mdogo.Familia yao ilipatwa na na matatizo na yeye alipofika walifurahi na kumpokea kwa furaha.Anapatwa na mtazamo kuwa labda matatizo yao yatapata muafaka na yatakuwa mazuri kwa siku za mbeleni.

Ghafla nyumba inaingiwa na mtikisiko na sauti nene ya vitisho ilisikika "Tunamgeni ? "  mdogo wake Sofia anapatwa na hofu na anakimbilia chumbani.Sofia anapatwa na hofu pia ila mama yake anampa moyo na kumwambia " hiyo ni sauti ya baba yako wa kambo usihofu".
Sofia anapungukiwa na hofu ila baada ya mda kidogo anasikia sauti ya mdogowake akipaza mlio na kupigwa.Mlio na kishindo cha kupigwa kikiandama nyumba yote.
Sofia alivumilia kwa mda wa wiki tatu na baadae aliamuwa kuhama na kutafuta mahala pengine kwa kuishi.Sehemu ambayo inaweza kuendeleza maisha yake kuanzia alipo na siku zake za mbeleni.

Uamuzi ni kuingia mtaani na kutafuta jinsi ya kuishiAlionekana msichana mdogo na mdhaifu.Watu walimpita na wengine walisema kuwa alikuwa maechanganyikiwa.Mazingira ya mjini yanamshinda kwani tofauti na yale ya kijijini. Anapaza sauti na kusema " Ni nini shetani toka mbele ya yangu na nitasonga mbele "  ghafla anatokea msichana mwingine na anamuuliza nini kimesibu na Sofia anamuuliza kwani wewe ni nani?

Yule msichana anamjibu yeye anaitwa tanya na anaweza kumsaidia kama anahitaji msaada.Tanya alikuwa ni msichana mrembo mwenye nguo za kisasa.Sofia alikuwa na nguo chakavu kwa wakati huo.Aliogopa kumjulisha Tanya kile kilichomsibu ingawa alikuwa na ulazimu kutokana na kutokuwa na mahala pa kulala kwa kipindi kile.
"Ninaitwa Sofia na nimgeni hapa mjini" alisikika kujibu Sofia huku akiwa na uso wa uzuni wenye mtiririko wa machozi.


Inaendelea. 

Haiusiani na picha iliyopo juu.

Kommentarer

Populära inlägg