uscuta

uscuta

Our Music online

tisdag 28 april 2015

Ni wazi kabisa kuwa sanaa ya Afrika ndiyo sanaa kongwe kuliko sanaa nyingine yeyote.
Sote tunajuwa kwamba maisha ya mwanadam yalianzia Afrika .Kumekuwa na kutokuamini kwamba Waafrika walikuwa mbele kisanii na kimaendeleo kabla ya kuanguka kwa tawala za kiafrika .
Utawala wa kiafrika ulijali mazingira ni utawala mabao hauja haribu mazingira kama tawala nyingine.
Kuna vigezo vingi tu ambavyo vinaonyesha kuwa Afrika ilikuwa mbele kimaendeleo ila hawakujihusisha na uchimbaji mafuta mfano petroli na madini kwa sababu walijuwa kuwa ni vitu ambavyo vinalinda mzunguko na uhusiano wa dunia na sayari nyingine.
Kuna mambo mengi ya kisayansi ambayo hayajangundulika kwa sasa ambayo yalikuwapo katika maktaba za waafrika wa mwanzo.
Kuna alama nyingi tu zinazoonyesha kuwa kulikuwa na watu wenye uwezo mkubwa wa kisayansi katika bara la Afrika.
Mfano mmojawapo ni kugundulika kwa sanamu ya Malkia Nerifetitti
Nilifanikiwa kuona sanamu hii nikiwa nchini ujerumani .Kuna kila haja ya kujifunza mengi ambayo yanahusu Afrika.                                                                                                                                   
Kuna jinsi watu wa nchi za magharibi wananufaika kutokana na waafrika kutotumia wataalamu wake kwa kisingizio cha kuwa waafrika ni wa mwishomwisho tu na hawajuwi kitu.Jiulize mwenyewe kama miaka zaidi ya Elfu tatu iliyopita tulikuwa na uwezo wa kufanya casting inashindikana vipi katika kizazi hiki cha sasa cha mwafrika?
Kuna ishara nyingi tu zinazoonyesha kuwepo kwa maendeleo Barani Afrika kabla ya kutawaliwa .
Mfano ni kugunduliwa kwa nyenzo mbali mbali za kufanyia kazi katika maeneo ya sahara.Nyenzo hizi zinaonyesha kuwa na umri mkubwa .
Afrika ni sehemu ya maisha katika sayari hii dunia. Kwa kuhariu mfumo wa maisha ya Afrika ni rahisi kuharibu mfumo mzima wa fikra na uelewa wa mwanadam na kusababisha majanga makubwa hapa duniani.   Anagalia mfumo wa maisha ya watu wa Afrika kusini .Inaonyesha watu wa Afrika kusini waligunduwa madini ya dhahabu kwa miaka mingi iliyopita kabla ya wageni kuwavamia .Inaonyesha kulikuwa na maendeleo makubwa katika Afrika kusini na watu wameanza kugunduwa majengo ya kale ya zaidi ya miaka elfu 2000 BC 
Inaonyesha kupandikizwa kwa watu kule Afrika kusini ni kujenga dhana mpya ya kuja kuleta matatizo ya mahusiano kati ya waafrika .
Kuna mengi ya kujifunza kuna mengi siwezi kuandika hapa ila unaweza kupata kwenye vitabu maktaba pamoja na tovuti mbali mbali.Nashukuru kwa kuwa umesoma na cha msingi ni kuelewa kuwa Afrika inahitaji kukombolewa ndipo watu wengine duniani wataishi kwa amnai na kurudi kwenye mfumo wa maisha yanayojali utunzaji wa mazingira  

Inga kommentarer:

Skicka en kommentar