Inajulikana kwamba kila mti una mwenzi wake .Kiufupi miti ina uhusiano wa namna ambayo mwanadamu hawezi kuelewa
Hapo zamani za kale kulikuwawepo na mti mkubwa uliokuwa umekaa peke yake kwenye macho ya mwanaadam.
Watu wengi walitamani kuutumia huo mti kwa kazi mbalimbali kama vile .ngoma za asili kuuza bidhaa n.k
Katika mti ule kulikuwa na kivuli kizuri kipindi cha kiangazi.Mti ulikuwa na upepo mwanana uliosindikizwa na sauti za ndege wa ajabu.
Watu wengi walifika mahala pale walijaribu kuuangalia ule mti na kusema ni vema wakapanda na miti mingine ili ile sehemu iwe na kivuli zaidi.
Walijaribu kupanda miti mingine lakini ilishindikana.
Wataalam kadhaa wa misitu walijaribu kuja na kudadisi ni aina gani ya miti ingweza kuota .Walijaribu kuipanda miti waliodhani ingeota ila haikuwezekana.

Siku moja kulikuwa na tamasha la ngoma usiku , Watu wengi walikusanyika kwenye ule mti mkubwa na kuanza kuburudika na ngoma iliyokuwa ikipigwa na kundi mahiri la ngoma.
Ghafla walisikia sauti nyingine ya ngoma ambayo hawakuitarajia .Ilikuwa ni sauti nzuri isiyoweza kuelezeka.
Ghafla waliona Mti umekuwa miti miwili na kuanza kuimba kwa sauti ya ajabu na ktk kila sauti iliingia kwenye mwili wa wale wanaadamu na kuwafanya waliwazike na kuwa na furaha isiyo na mfano.
Ghafla tena waliona miti midogomidogo ikicheza kuzunguka ile miti miwili mikubwa.

Tokea hapo watu wa kijiji waliupa jina ule mti na kuuita Mti unaotembea.


Kommentarer

Populära inlägg