Uhakika wa msanii




Kuna njia nyingi za kufanya kazi ya sanaa .Kuna wale wanaohitaji kujua njia moja tu na kuifanyia kazi vizuri na kuna wale wanaohitaji njia nyingi na kufanyai kazi moja vizuri.
Sanaa ni maisha ya mwanadamu ya kila siku yanayoakisiwa na msanii.
Kwenye maisha ya mwanadamu huwa na uchunguzi wa kila namna ili kuyatambua vizuri maisha yake.Nasema hivi kwani wasanii wengi wa kiTanzania wahajapewa nafasi ya kuyambua na kuyafanyia majaribio maisha yao.
Kuna namna nyingi za kuyafania majaribio maisha.Kuna njia ya kisayansi na njia ya kawaida ya kijamii tu.
Kwenye njia ya kisayansi mwanadamu anatakiwa awe na uhakika wa kimahesabu wa kile anachokifanya hapa Duniani.
Mfano ni plae mwanadamu anapotoa hoja ya ujenzi ,ubunifu ramani ,hoja ya kibenk n.k
Msanii pia anaweza kufanya sanaa ya namna hii ambayo ina majibu ya asilimia mia moja lakini kwa upande wa pili atakuwa ameibana au kuiweka sanaa yake kwenye hukumu kubwa kutoka kwa washabiki pamoja na
wajuzi wa kazi ile anayoifanya.
Mfano mzuri ni pale msanii anapotaka kuchora picha halisi ya ,mwanadamu, wanyama mfano Tembo ,Simba Twiga n.k
Kuna mabo mengi ya kuangalia nje ya upakaji wa rangi nzuri.Hii ni kutokana na kuwepo na fotokop mpaka za kukopi picha kuwa sanamu halilisi.
Kuna washabiki wanaopenda mpangilio wa perspective (mwonekano) yaani mpiga picha alikuwa wapi na je maumbo ,kivuli au vivuli vinakubalika kwenye upeo wa macho?

Msanii atakuwa amejiweka kwenye nafasi ngumu pale atakapokuwa ameshindwa kuwakilisha kimoja ya kile alichokusudia.
Mfano msanii anadhani miguu yote ya Tembo imekaa sawa wakati washabiki wanaona kinyume.
Kwa washabiki wa nchi zilizoendelea wanaona picha nyingi kubwa na za kisasa kwa hiyo ni vigumu kuwadanganya ukilinganiasha na wa ki Afrika.
Mimi binafsi napendelea sana kuona ubunifu wa Rangi zaidi ya maumbo pale ninapoangalia Mchoro wa rangi ( painting)
Rangi ina mengi ya kuelezea ukilinganisha na maumbo.
Rangi huleta maumbo ya kuhisi ambayo kila msanii anayo ,na maumbo ya kuhisi yanaweza kuleta picha halisi baada ya uchunguzi.
Napenda kusema kwamba , watoto wadogo wamekuwa wakiwasilisha sanaa ya upakaji rangi zaidi ya watu wazima wa karne hii.
Najuwa kuwa sanaa ya Tanzania imearibiwa sana na soko la ununuzi la watalii.
Sanaa haitegemei watalii ,ila watalii wanategemea sanaa.
Isiwe rahisi kwa msanii kuharibu ujuzi wake kwa kutegemea sana sifa ama fedha za ununuzi wa kazi kwa lengo la kuwauzia watalii.
Kipato cha msanii kinaweza kuwa kikubwa kwa kutegemea soko la ndani. Mfano tunaona kwenye mziki ,filamu n.k
Mmbando Kennedy
Language Kiswahili
chaooo
Itaendelea :)

Kommentarer

Populära inlägg