Ilikuwa kwenye mwezi wa kumi siku ya ijumaa kutokea kwenye usiku wa Jose Chameleon alipotumbuiza kwenye jiji la Stockholm .Ilikuwa ni usiku wa pamoja wa watu kutokea Afrika mashariki.
Kama tunavyojua Afrika mashariki inajumuisha nchi za Uganda ,Rwanda ,Sudan ya kusini ,Burundi ,Kenya na Tanzania.
Kitu kikubwa kilichokuwa cha pekee ni pale wasanii walimsindikiza Jose Chameleon ikiwa ni pamoja na msanii wa Reggae kutoka Tanzania Dabo na wengine wanaoishi Sweden.
Kwa kweli inaonyeesha ni jinsi gani kuna vipaji vingi sana vya wasanii wa Afrika mashariki ukizingatia wote walijaribu kuimba kwa lugha ya kiswahili .
Wasahbiki wengi waliofika mahala hapo walipendezwa sana .
Picha chini ni Kennedy akiwa pamoja na shabiki wa Jose kutoka jijini Stockholm
Kommentarer
Skicka en kommentar