Jana tulifanikiwa kumaliza video ya Musik Mrembo

Baada ya kumalizia nyimbo za album kazi iliyobakia ni kutengeneza video katika nyimbo zote tulizofanya.
Shukrani za dhati ziwaendee Pappa herimit kwenye kamera pamoja na Tommy fröjd kwa kumix nyimbo na kufanikisha kazi ya hii Album My Wrld of Art by Kennedy.
Kitu kilichofurahisha kwenye album hii ni jinsi muunganiko wa alla na sauti za asili haswa kutokea Mashariki mwa Afrika Tanzania ,Uganda ,Kenya ,Rwanda ,Burundi n.k zilivyotumika kwa ufasaha na zinaweza kukufanya utulize akili pindi unaposikiliza hizi nyimbo.
Ni matumaini yetu kwamba mtatupa ushirikiano mzuri ili tuweze kupata views za kutosha kwenye
Spotfy.
Shukran
// Mmbando Kennedy

Kommentarer

Populära inlägg