Amanina Upendo






Mwimbo huu unahusu kushirikiana na kuwa na upendo baina yetu hapa duniani. Nimemshirikisha PappaHermit kutoka marekani ambaye ameweka maneno mepesi kwa kiswahil. Kama mnavyojua lugha ya kiswahil imekuwa maarufu Marekani pamoja na dunia kwa ujumla kwa hiyo ni fursa kwa sisi wasanii kufundisha kiswahil kwa njia ya utenzi wa mashairi . Ni matumaini yangu mtausikiliza huu wimbo na kutupa sapoti ya nguvu ili tuweze kuuza album yetu kwenye Spotfy na maduka mengine kadhaa . Uzuri wa kufanya kazi kama hizi ni kuonyesha kuwa tuna heshimu na kujivunia tamaduni zetu pia kugawana mawazo mbalimbali mazuri kwa njia ya mziki. Nimekuwa nikichanganya mziki wangu na kujaribu kuweka sauti halisi katika hisia mbalimbali haswa za kienyeji kwa sababu ya kukumbuka uhalisia wa sauti mbalimbali za waswahili haswa sauti yangu ni ya aina yake . Nikiwa bagamoyo nilipata nafasi ya kushiriki masomo mbalimbali ya kuendeleza mziki wetu huku tukilinda uhalisia wetu. Asanteni sana kwa kusiliza nyimbo yetu Nyimbo AMANI NA UPENDO ARTST KENNEDY MY FT PAPPAHERMIT PROD FRÖJD BGS STUDIO www.kennedym.com

Kommentarer

Populära inlägg