Mmbando Kennedy drawing

Ninashiriki kwenye maonyesho ya Twitter Art Exhibit: Los Angeles!
Nimeamuwa kufanaya kazi ya kutoa shukrani kwa wale wote waliosaidia wengine kwenye mwaka 2012 .
Kuna malalamiko mengi kuhusu watu kujisikia kuchoshwa na kusaidia bila ya kupewa shukrani au bila ya waliosaidiwa kuonyesha kushukuru kwa msaada waliopata.
Binadamu tumekuwa na tatizo kubwa la kati wanaosaidiwa na wanaosaidia.
Dunia ingekuwa mahala pazuri kama watu wote wangeweza kuwa na moyo wa kuona kuwa msaada wanaopata si lazma na inabidi washukuru kwa kiwango fulani.
Shukrani ni jambo la bure ingwa linatokea moyoni.Dunia inaweza kuwa mahala pazuir pa kuishi kama tu watu wangejuwa kuwa kusaidiwa si kudhalilishwa na kujuwa umesaidiwa ni moja baraka na inaweza kusaidia yule aliyesaidiwa kusaidia wengine.
Kuna wanadamu wengine wamepanga kutosaidiwa na labda wakisaidiwa lazma na wao wawe wametangazwa kumsaidia yule aliyesaidia ndipo wajisikie vizuri.
Ikitokea kuelemewa upande mmoja basi inaweza kusababisha matatizo kwani aliyesaidiwa anaweza kuanza kumuhujumu yule aliyemsaidia bila ya kujuwa.
Katika bara la Afrika kumekuwa na tatizo kubwa kati ya matajir na maskini.
Matajiri wengi wamekuwa wakiepuka kusaidia maskini kwa hofu ya kudharauliwa.
Baada ya hapo kukazaliwa tabia ya matajiri kujilinda na kuanza kuwa pangia maisha ya umaskini wale wanaohitaji kusaidiwa wengi wao wakiwa ni mskini.
Tunapaswa kujuwa kuwa watu wote wanahiataji kusaidiwa iwe ni tajiri ama maskini.
Upendo wa mwanadamu upo kwenye kusaidiana na anayesaidiwa akiona amefanikiwa basi anatakiwa ashukuru pia asaidie wengine.
Ipo misaada ya aina nyingi kimawazo na kimwili.

Kommentarer

Populära inlägg