Matukio Ghafla.
kwenye meli
mazungumzo na vijana
chakula kizuri
kuhusu kuwa na pasipoti kwenye safari
ndani ya
Rap kwa ufupi
Ilikuwa ndani ya meli tukiwa tunasafiri
kwa ajili ya mapumziko mafupi.Kulikuwa na watu wengi na wengiwao ni
watoto na wazazi.
Vijana wengi walionyesha kuwa na
mtazamo tofauti na ule wa wasichana ingawa wasichana walikuwa
wanalewa na kujaribu kujificha na kulewa zaidi.Vijana walikuwa
wanatumia vitambulisho vya kaka zao kwa ajili ya kununulia pombe na
kisha kujificha na kunywa na wasichana.
Niliamuwa kuzungumza na kijana wa
kwanza.Kijana alisema kuwa yeye anasafiri na mama yake na alianza
kulaumu matokeo ya vita ya wenyewe kwa wenyewe kule nchini kwao
Mashariki ya kati.
Alianza kwa kusema , kaka angalia jinsi
walivyokuwa wajinga wanauwa vijana wadogo hata kabla hawaja fumbuwa
macho yao.Hii ni jinsi alivyokuwa anaizungumzia nchi ya Sirya.
Aliendelea kulaumu jinsi nchi za
magharibi zinavyojihusisha kwenye migogoro yao na kwa madai ya kwamba
wapo kwenye biashara ya mafuta.
“wanaanzisha migogoro Sirya kwa ajili
ya kupata njia ya kuchukuwa mafuta ya Iraki” aliendelea kusema.
Tulikuwa tunaongea na ghafla tukaletewa
chakula.Chakula kilikuwa kizuri sana na kijana aliendelea kwa kusema
anampenda mfalme wa Sweden kwa sababu anajali watu wake.
Angalia myronna ni sehemu ya kuweka
nguo zilizochakaa kidogo na kisha kuwasaidia watu wasio na
uwezo.Aliniuliza kama na sisi tunafanya hivyo kule Tanzania na
nilimjibu hapana.
Kwa haraka niligunduwa na sisi
tulipaswa kufanya hivyo kwani tuna watu wenye uwezo wa kubadilisha
nguo kila mwezi na si wangeweza kuzi gawa nguo za zamani kwa watu
wasio na uwezo? Nilienedelea kujiuliza.
Ghafla tulielekea kwenye sehemu ya juu
ambapo kulikuwa na vijana wengi wakicheza mziki,wengi wao walicheza
na wazazi wao.Kijana niliyekuwa nae alianza kucheza na ghafla alianza
kucheza na watoto wa kike walio sawa na umri wake.Ghafla mzazi mmoja
laimuuliza kwa nini anacheza na wale watoto wenzie na kama anaweza
kujuwa kuwa wao ni watoto.Yule kijana akamjibu alikuwa anacheza na
wale watoto kwani na yeye alikuwa mtoto pia.Nilimuuliza alikuwa na
miaka mingapi na alijibu mikaka kumi na sita.Na kweli wale vijana
wengine walikuwa na mika kati ya kumi na sita mpaka saba.
Aliendelea kusema kuwa yule
aliyemuuliza akupenda kumuona anafuraha kwani alikuwa nanonekana kwa
sura ya kiarabu.
Nilimshauri kutulia na ni vizuri
akaenda kukaa na wazazi wake mpaka hasira zitapopunguwa.Najuwa kuwa
inauma kuona upo kwenye nchi yako na unapangwa kwenye makundi
kutokana na muonekano ulio nao.
Kijana alienda kuonana na wazazi wake
na hakurudi mpaka tulipokutana kesho yake.
Ghafla walikuja rafiki zake .”hi
brother “ walisema na mimi nikawajibu “hi” waliendelea
kuniuliza kama ningewaimbia baadhi ya nyimbo mfano Bob Malrey
,Eminemy ,J Z,0 Cent na nyingine nyingi.
Niliwajibu ninaweza kama nina maneno
yao ila ninapendelea kuimba nyimbo zangu mwenyewe.
Waliniomba niwaimbie na nilianza kwa
kurap nyimbo kadhaa.
Waliniuliza kama nyimbo zipo kwenye Tv.
Leo ni siku ya ijumaa na nimeendaz
Upsala kwa ajili ya kesi ya madai ya ugomvi kati yangu na watu
kadhaa.Nimeamuwa kusoma baadhi ya vitabu vya sheria ili kuona ni
jinsi gani ya kuelezea tukio.
Kumekuwa na matatizo ya kubakikiwa kesi
kwa watu wenye asili ya ugeni,nimeamuwa kusoma sheria zao ili nielewe
na kuamuwa kujilinda na kulinda jamii ya waafrika
wanaiokuja.washichana wengi wametumia sheria ya unyanyaswaji kwa
ajili ya kujiingizia kipato haswa kwa watu wageni wasiojuwa sheria
zao.Tumekuwa tukinyanyaswa kwa namna moja au nyingine juu ya kuwa
sisi ndiyo wenye kosa hata kama si sisi tumetenda kosa.
Wadada wawili wanatoka kwenye basi
,wanaanza kurumbana na bibi mmoja aliyekuwa anazungumza na mimi.
Nilipowauliza ni kwa nini wanamtukana
yule bibi walianza kunitishia uhai kwa kusema watanivamia .
Ghafla ulianza ugomvi na mimi nilipigwa
chupa mkononi na mkoni uliumia.Watu waliokuwa pale walionyesha
kunichukia na ghafla walikuja polisi na kunikamata.
Niliwauliza ni kwa nini na walishindwa
kueleza sababu.Walikuwa wanasema nimelewa wakati sikuwa nimelewa.
Niliwekwa kituoni mpaka
asubuhi,ilipofika asubuhi niliojiwa na dada mmoja mwenye nguo za
Polisi ,aliniangalia mkono na aliona umeteguka.
Niliamuwa kwenda Hospitali na
nikafanyiwa uchunguzi kwa njia ya e ray.Daktari aliamuwa wanifanyie
opasuaji.
Nilifikiri inaweza kuwa njia ya
kuharibu mkono wangu kwani ndiyo ninaofanyia kazi.Niliamuwa kwenda
Stockholm .Niliwasiliana na watu ninaofanya nao kazi .Walinisaidia
kunipeleka kwenye ospitali ya mjini Stockholm.
Nilionana na daktari mwingine na
alinifanyia uchunguzi kisha akasema atajaribu kuninyoosha mkono
na nisingehitaji upasuaji.
Nilifanyiwa unyyoshaji na kisha
nilienda nyumbani .Nilirudi kwa daktari baada ya wiki mbili na
aliniangalia tena na kuninyoosha mkono na nilirudi tena baada ya wiki
mbili na kutolewa ogo.
Nilipewa msharti ya kufanya Mazoezi na
baada ya mda nilipona.
Kwenye ndoto kuna mambo mengi ya msingi
na nimeamuwa kufuatilia na kulinganisha ndoto na hali alisi ya
kawaida ya mwanadamu.Matukio mengi ya kwenye ndoto yanalinga na ya
hali halisi ya mwanadamu wa kawaida.
Kuna watu wamesema tupuuzie ndoto hali
kwamba ndoto inakubalika hata mahakamani.Kuna watu wameota matendo na
kuthibitisha katika hali ya kawaida.
Najaribu kelezea ndoto kwenye michoro
yangu na nimekuwa nikiweka alama zote zinazotokea kwenye ndoto.Najuwa
kwamba ninakazi kubwa ya kuchora yote yaliyo tokea kwenye ndoto kwani
ni mengi na yote ni ya maana.
Moto mkubwa unatokea kwenye mkono na
ghafla najitaidi kuangalia na ninaona ni moto mkali na unanagaa zaidi
ya almasi.Sauti inasikika ikisema tumia nguvu uliyonayo ,unanguvu ya
kufanya maajabu .Najiuliza kama nimeshatumia nguvu na najuwa kuwa
nimekuwa nikidharau na kupuuza nguvu iliyo ndani yangu.
Nimekuwa nikijenga furaha kwa watu
wasiona umuhimu kwangu na kuwaacha wale walio na umuhimu.
Watu wa Mungu ni wengi na wenye furaha
,tumekuwa tukijihusisha kwenye matendo ya kuridhisha watu wasio na
mapenzi ya kweli.Tumepoteza mda mwingi kuwaridhisha watu wasiotosheka
na fadhila.
Taifa la Mungu linatuhitaji ,kweli ya
kweli idumu kwa walio na kweli ,maji chumvi na maji sukari
hayashikamani
Naamka na nasikia sauti ikisema
,nasikiliza na kuthibitisha ni sauti ya kweli na inasisitiza juu ya
kutumia nguvu kubwa ya maajabu.Najiuliza na naona mwanga mkuu kwenye
mwili unaangaza na unapotelea ndani ya mwili.
Nguvu kuu ni ya maajabu , nguvu kuu ya
kuhamisha milima na miji mikubwa na kupeleka kwenye sehemu za
mapambano.
Nguvu kuu ya kutikisa miji mikuu na
kuangaza sehemu zenye giza.Nguvu kuu ya kutikisa walio na uwezo wa
kishetani na kuwaelekeza kwenye Upendo wa mwenyezi Mungu.Nguvu kuu ya
kulinda na kuhifadhi vile vyote vyenye kuheshimu na kulinda haki ya
mwanadamu.
Haiitaji kumgusa mtu na kufanya miujiza
kwani miujiza haina mipaka.Tunafanya miujiza duniani na hata kwenye
mbingu.
Ni vigumu kuamini kwenye jambo lenye
ukweli .Kwenye mwanga kuna mwanga na mstari kwenye mwanga na ncha ya
mwanga kuwa mwanga na giza kupambana na mwanga.
Kitabu chao cha wenye kudhani wanauwezo
kinageuka juu chini nikiweka kitandanai kwangu,ishara ya juu chini ni
ishara ya kuonyesha nisiamini mambo wanayonifunza na nianze kufuata
na kufanya mambo yangu.
Wao wana jaribu kutafuta nguvu uliyo
nayo ili watumie kwa ajili ya jamii yao na wewe unanguvu kwa ajili ya
kukomboa jamii yako.
Kuna uwezo wa kuchasaidia wenzetu ila
si kwa njia ya kutudanganya na kuchukuwa kila tulicha nacho kwa faida
yao binafsi.
Nilikuwa na rafiki zangu tukiimba na
nilikuwa naimba kwenye jukwaa lenye watu wengi wa kila aina.
Natumia nguvu ya miujiza na rafiki
yangu mmoja aligunduwa na tuliimba kwa pamoja.Wengine watatu
walijaribu lakini walishindwa .Tuliimba na kuendesha baiskeli
jukwaani .Niliwasikia wakinongona na kujiuliza tulipata wapi
nguvu.Watu wengi walishangilia na tulipata wafuasi wengi.
Niliona watu wa zamania niliosoma nao
upande wa pili ,baadhi ninawakumbuka na baadhi siwakumbuki.Kuna
waliofurahishwa na waliojiuliza ,wengine walijaribu kufananisha ila
walishindwa.
Kundi kubwa la watu lilitufuata na
tulipanda gari na kuelekea makwetu.Nilimfundisha rafiki yangu lugha
ngeni na tulitumia kwenye nyimbo ,watangazaji wengi walifurahishwa na
tunzi zile walijaribu kuwasiliana nasi .
Sfarini kwenda Finlandi na boti ya
Silja.
Tulifika kwenye mapokezi ya biti mapema
na mimi na mwanangu Isaki tulikaa kusubiri turuhusiwe kuingia ndani.
Joyce na Rikard walikuja na watoto zao
Arvin na Arvid pamoja na dada yake Joyce.
Tulianzan safari saa kumi na mbili
jioni.watu wote waliingia kwenye Boti na walionekana kuwa na furaha
wakubwa kwa wadogo.
Tulienda kununuwa vitu vya kula kwenye
duka na baadae Tulienda nje kwenye maonyesho mbalimbali.
Kulikuwa na bendi ya mziki mwanana
kutoka Brazil na watu wengi waliangalia michezo yao ya kapoera pamoja
na mwimbaji wao mashuhuri wa kike.
Tulizunguka boti nzima niliona vijana
mbali mbali wakiwa wamechoka kutokana na kunywa pombe sana.
Tuliwapeleka watoto kwenye bwawa la
kuogelea na walifurahi sana.
Hamna kitu cha umuhimu kwa watoto kama
kucheza na mumi na kucheza kwenye sehemu za kuchezea watoto na kisha
kwenda kuogelea.
Nakumbuka sisi watoto wa kiafrika
hatukuwa na sehemu kama hizi kwa kipindi tulichokuwa tunakuwa kwenye
miaka ya themanini.
Nakumbuka siku moja ilitugharimu
tutafute sehemu ya kychezea na tulizunguka eneo kubwa na tuliishia
kuokota silaha badala ya kupata sehemu ya kuchezea.
Wtoto wanahitaji kupata sehemu za
kuchezea ili kuweza kutumia mda wao wa utoto kucheza na kuongeza
ujuzi.
Afarai ya basi Swedbuss
Ilikuwa siku ya jumapili baada ya
kumrudisha mwanagu nyumbani.Tuliamuwa kurudi nyumbani jumapili baada
ya safari nzuri ya boti.
Nilipata usafiri wa Swed bus ni safari
nzuri kwa kuwa wanamabsi mazuri .Nimekutana na watu wengi wenye
kuoneka kama wametoka kwenye sherehe mbali mbali siku ya jumapili na
sasa wanaamuwa kurudi manyumbani kwao.
Kunauwezekana mkubwa wa kusafiri na
mabasi kwa hali nzuri ya kuonekana mtalii ikiwa tu mabasi yanuwezo
mzuri na yamejengwa kwenye ubora unaotakiwa.
Usafiri wa mabasi hapa ni mzuri sana
kwa sababu mabasi yanaubora wa kiwango cha juu ukilinganisha na
Tanzania ambapo kuna matatizo makubwa kwenye huduma ya usafiri.
Wawekezaji wa nchi maskini hawajali
ubora wa huduma wanazotowa kwa kuwa wamekuwa wakitumia vifaa
vichakavu na wamekuwa wakihatarisha maisha ya wasafiri wengi ikiwa ni
pamoja na watalii kutoka nchi mbali mbali.
Tunapishana na magari mbali mbali yenye
kuonekana tufauti tofauti.Magari mengi ni ya familia na yanaonekana
kuaharakisha kutokana na watu kwenda makazini kesho.
Watu wengi wanatumia siku za mwisho wa
wiki kutembelea familia zao huku wengine wakitumia magari binafsi.
Usafir wa magari binafsi ni mzuri pia
kwa watu wasiotumia vilevi.Ni usafiri wa kuharakisha harakisha kwa
wale wanaotumia vilevi.
Napenda kutumia mabasi kwa sababu
hayaharakishi yanapokuwa njiani na yanafuata ubora na matakwa ya
Abiria.
Tunapita kwenye misitu karibia na
Arboga na tuanaona nje kunakuwa na giza nene kutokana na wingi wa
misitu.
Misitu ya nchi za skandinavia ni ile ya
kupandwa na inaonekana kufanana.Ni misitu yenye matawi madogo ila
imebanana kwa hiyo ni vigumu kupitisha mwanga.
Najuwa kuwa kuna giza jingi wakati wa
kipindi cha baridi na mwanga mwingi wakati wa kipindi cha kiangazi.
Kumekuwa na vifaa vingi vya kuakisi
mwanga barabarani kipindi cha baridi ili waendesha magari yaweze
kuona kule yanapoelekea.
Ok , niwakati wakutambuwa na kuelewa
tunaishi na viumbe wa aina mbali mbali .Moja wapo ya njia ya
kuwatambuwa ni kujuwa jinsi wanavyofikiri na kurekodi matukio
wanayofanya.Nimekuwa nikitakia mema jamii yangu na ninaelewa
inawezekana kujaribu kufanya jambo la umuhimu kwa pamoja kama mambo
haya ninayoyaona hapa.
Miundo mbinu ni moja ya mtego
uliokuwepo kwenye karne hii ya 21 .Watu wengi wanaingia kwenye
matatizo ya kuchanganya matukio mbilimbali huku wakidhani ni
mabadiliko ya kisayansi
Kuna vijana wengi wanakumbwa na tabia
ya kufanya mambo yasiyo na mwongozo huku nchi nyingi haswa za bara la
Afrika zinamigogooro ya kijamii pamoja na mabadiliko ya kisayansi.
Kumekuwa na trik wanayoifanya waandaaji
wa huu utumwa mamboleo haswa kwa jinsi walivyobadilisha mazingira ya
kimasaa pamoja na jinsi watu watakavyofanya kazi zaidi ya mda maalumu
walioupanga.
Watu wengi wamejichanganya na uovu wa
shetani kwenye nyumba za kawaida mpaka nyumba za ibada.
Najuwa inakuwa vigumu kuelezea jinsi
mtu anaweza kujuwa anachohitaji kufanya na jinsi ninavyoona wao
wanavyopanga ingawa kunauwezekano wa kugunduwa kwa uwezo wa roho
mtakatifu.
Fikiria jinsi mazingira yanavyoharibiwa
na wale waliovaa ngozi ya ubinadaam.Wasiyojuwa hili wanakaa chini yao
na kuharibu ndugu zao kwa msingi wa kutetea kile wanachojuwa wao.
Kumekuwa na miradi ya kuuwa kile
kinachotufanya tuwe wanadaamu na kupromoti au kutangaza kile kisicho
na uhai na uanaadam.
Najuwa wengi wanachukia kwa kuwa
wanaukweli ndani ya mioyo yao.Wanajuwa wanachokifanya na kwa uelewa
wa wasiojuwa wanawatumia kuharibu vile vizuri tulivyojaliwa na
mwenyezi Mungu.
Mungu ni upendo na upendo wa kweli usio
na mwisho wala mwanzo.Ni vigumu kuelezea kwa lugha ya kawaida
.Unatakiwa utambuwe kweli iliyo huru na ujuwe heshima yetu kwa muumba
wetu ni ufunguo wetu wa kuishi maisha matakatifu.
Kumekuwa na mvutano wa watu wema na
wabaya na kumekuwa na mchanganyo wa kufanya mambo matakatifu kwenye
mambo yasiyo matakatifu .
Binadamu anaishi na shetani kwenye
mazingira ya mkataba wa siku hizi za mwisho.Binadamu amesaliti
matakwa ya mwenyezi Mungu na kuingiza matakwa yake na ya shetani
kwenye maisha ya kawaida ya binadamu.
Hii ni kosa kwa sababu kwa nini Matakwa
ya binaadamu na yashetani yanakubalika kwa urahisi na si matakwa ya
Mungu.
Kumekuwa na kutokukubaliana na mambo
mema tokea zambi ya kwanza aliyofanya mwanadamu.Mambo mema yanatumiwa
kama mabay na mabaya yanatumiwa kama mema.
Kommentarer
Skicka en kommentar