Sijeme na Sofia.
Ilikuwa katika pilikapilika za mjini ndipo Sofia alikutana na kijana Sijeme.
Sijeme alikuwa ni mmoja wa vijana waliokulia maisha ya mtaani ingawa alifanikiwa kusoma na kupata kazi usalama wa Taifa.
Sijeme ni mmoja wa wafanyakazi hodari katika idara yake.
Walianza kwa kusalimiana huku wakiwa hawaamini macho yao.
Sijeme: "Siamini Macho yangu"
Sofia: " Usihofu milima haikutani Binadamu hukutana"
Sijeme; Unamda tukae kwenye mgahawa na kuzungumza zaidi.
Sofia: Haina Shaka .
Waliingia kwenye mghahawa na kuanza kuzungumza.Sijeme alinunuwa chakula kitamu na cha kuwatosha wote wawili.
Alimuangalia Sofia mara kwa mara na aligunduwa kuna kitu kinamsibu Sofia.
Sofia alijaribu kujikaza na kuficha hisia zake lakinihaikuwezekana.
"Ni nini kimekusibu " Aliuliza Sijeme
Sofia alielezea mkasa mzima uliotokea pindi walipoachana wakiwa wadogo pale mtaani.
Sijeme alishangazwa na kitendo alichofanyiwa Sofia.
"Unakumbuka anapoishi ? " Aliuliza Sijeme
"Ndiyo" alijibu Sofia
Ghafla Sijeme alimpakia Sofia kwenye gari na kuelekea Kule alipofanyiwa unyama sofia.
Kiza kinene.
Mahojiano na Polisi:
Polisi: Unajuwa wewe ni Afisa usalama? Kwa niniumefanya haya yaliyotokea?
Sijeme alikuwa kimya.
Polisi : NAKAJI UNIJIBU UMESIKIA ?
Sijeme : ndiyo
Polisi :Unakumbuka uliyofanya ?
Sijeme:Ndiyo
Polisi: Kwa nini umefanya ?
Sijeme alielezea mkasa mzima .
Sijeme alikuwa mtoto wa mtaani kwa sababu baba yake aliuliwa na mmoja wa afisa mkubwa serikalini .Kitu cha kushangaza ni afisa huyo ndiye alimbaka Sofia Pia.
Sijeme alisomea usalama huku akifuatilia na kujuwa wale waliohusika na kifo cha baba yake.
Ilikuwa vigumu kujizuia kwani alikutana na adui yake ambaye ameharibu maisha ya Sofia huku alitaka kuharibu maisha yake pia.
"Ni nini kingefanyika ?" Aliuliza Sijeme huku akimwangalia Polisi
Kommentarer
Skicka en kommentar