Refugees right is important

Kuna msemo unasema wakimbizi wanakimbilia kule watakapoweza kupewa uhuru wa kuzungumzia ni nini wanahitaji ili waweze kurekebisha hali ya maisha ya kule walipo kimbia iwe walikimbia vita au la. Mkimbizi ni nani? Mkimbizi ni mtu ambaye amelazimika kukimbia nchi yake kwa sababu ya mateso, vita au vurugu. Watu hawa wana hofu ya msingi ya mateso kwa sababu ya rangi, dini, taifa, maoni ya kisiasa au uanachama katika kundi fulani la jamii. Uwezekano mkubwa, hawawezi kurudi nyumbani au wanaogopa kufanya hivyo kuepuka Vita na ukatili wa kikabila,wasiwasi na tofauti za kidini ni sababu za wakimbizi wanaokimbia nchi zao.Kuna aina nyingi za ukimbizi ila kubwa ni hizi 1.Wakimbizi wa kivita. 2Wakimbizi wa kiuchumi 3 Wakimbizi walioathirika na Mazingira (dhoruba) 4 Wakimbizi wa matatizo ya kiuwanawake 5 Wakimbizi watoto waliotoroka familia au kutoroshwa 6 Wakimbizi wa hifadhi n.k Inasemekana katika maisha ya kawaida kila mwanadamu amekuwa mkimbizi tokea Binadamu wa kwanza walipo hasi maisha yao kule bustani ya Aden.Kwa hiyo utaona binadamu amekuwa akipambana na changamoto za maisha ya eneo alilopo na yakimshinda huwa anategemea kubadilisha mazingira na hii inaweza kuwa ni kwa hali ya kawaida au hali ya kikimbizi. Tumekuwa tukiona baadhi ya watu wakikimbia makazi yao na kuhamia wasipopajua.Watu hawa wamekuwa ktk maisha mapya yasiyo na matumaini.Katika hili familia nyingi zimepoteza wanafamilia haswa watoto na vijana . Unaweza kujiuliza kwanini tunapaswa kujali maisha ya wengine na tusiendelee kuishi tu maisha ya yetu ya kawaida? Najuwa kuna watu wanaumia sana wanaposikia wakiongelewa wale ambao hawawezi kujitete au la.Ukweli ni kwamba utafiti wa shirika la UNHCR linaonyesha kuna idadi kubwa ya wakimbizi waliokimbia makazi yao kutokana na vurugu za kivita. Nimetengeneza hii nyimbo nyimbo na kuandika maneno haya ili kuonyehs umuhimu wa kujali maisha ya wengine ,kutunza mazingira kuepuka na vita n.k Naamini Mungu ameumba dunia sehemu nzuri na tunayonafasi ya kutumia ujuzi na busara tulizonazo kujenga jamii badala ya kubomoa na kuleta maafa. By Mmbando Kennedy 2019 #uscuta2000 www.kennedym.com

Kommentarer

Populära inlägg